Saturday, November 05, 2005

Watazamaji Hawa Waliona Uchaguzi Upi?


Eti uchaguzi Mkuu Zanzibar ulikuwa Huru, Haki na Tulivu! Maajabu.
Inashangaza kidogo, kuona uchaguzi wa Zanzibar uliotwaliwa na kasoro nyingi, vurugu na uvunjaji wa haki za binadamu hasa wa upinzani, KAMA HIVI unapoitwa huru na haki, na kuwa ulifanyika katika mazingira ya amani na utulivu. Soma hapa uone matokeo ya uchaguzi huo. Na hapa kuna mambo zaidi. Cha ajabu baadhi ya watazamaji wa Kimataifa na wengine wa ndani wamesema ulikuwa huru na haki, lakini Hapa Marekani imekataa kuafikiana nao, CUF nao wamo, lakini wote wametofautiana na Serikali ya Zanzibar. Soma hapa kwa maoni yangu binafsi. (Kulia ni gari laalum la Polisi likiwamwagia wakazi wa Zanzibar maji yanyowasha kama upupu. Walioyaona wanasema yana rangi nyekundu)

2 comments:

Mija Shija Sayi said...

Isijekuwa waliokimbilia msituni wameenda kujifua sisi tunabaki kudhani wanakimbia kamata kamata.

Ndesanjo Macha said...

Picha hii nzuri sana. Ni kielelezo cha huo uchaguzi "huru na wa haki" wanaotuambia hawa "waangalizi" wanaolipwa maelfu ya dola za Kimarekani. Uchaguzi wa huru na haki unafahamika bila hata hao waangalizi.

Post a Comment