Saturday, October 08, 2005

Mchezo gani huu wa kurudi nyuma

Haya ndiyo mambo gani? Mchezo gani huu? Pengine ni maswali ya kila mmoja kujiuliza. Wakati upinzani unaendelea kupata nguvu, na Chadema kuvuna wanachama na hisia za wananchi, yanatokea kama haya. Mmoja wa makada wake anaamua ' bila shaka ameamua mwenyewe' kurudi CCM. Ameacha Uenyekiti wa Mkoa wa Chadema na kubwaga manyanga katika kinyang'anyiro cha ubunge katika Jimbo la Morogoro Kusini. Kama Picha hii ya Daily News na maelezo yake hapa chini inavyoeleza:
CCM Union presidential candidate Jakaya Kikwete shakes hands with the former Morogoro Regional Chadema Chairman, Mr David Mgesi, who was also parliamentary candidate for Morogoro South Constituency in Dar es Salaam yesterday. Mr Mugesi told a news conference at the CCM sub-head office along Lumumba Street in the city that he was joining CCM. (Photo by Semu Mwakyanjala) Lakini, vyombo vya habari vimeelezea tukio hilo kwa namna tofauti. Soma hii http://www.kurayako.com/2005/habari/article.php?cmd=view&article_id=305 na hapa Freeman Mbowe, Mgombea Urais wa Chadema akijibu hoja ya kutumia helkopta: http://www.kurayako.com/2005/habari/article.php?cmd=view&article_id=283

1 comment:

Anonymous said...

kama chadema wanachukua mapesa toka uingreza kama makala hiyo inavyosema mie natia walakini. Kumbe ndio maana wanaweza kukodi helikopta kuwahadaa masikini... wabongo wanakuja kuangalia helikopta au kusikiliza hoja za mgombea?
Pesa za kufadhili wagombea zitoke kwa wananchi wanaopenda chadema.Muingereza, tena conservative! aipende tanzania? au chadema? thubutu!!
Angalieni tusiwe tunawatengeneza akina Tzvangirai wa MDC ya Zimbabwe. pesa zote wanapata kutoka uingereza... wanatia karaha tupu..

Post a Comment