Sunday, January 16, 2005

Makao Makuu 'Yakaribia' Kuhamaia Dodoma

GESTI 'nyumba za kulala wageni' zinaendelea kukarabatia na mpya zinaendelea kujengwa. Baa zinapanuliwa na kuongezeqwa viti. Maeneo ya nyamachoma yanaadaliwa kwa ajili ya tukio. Tukio lenyewe, si jingine bali ni makao makuu ya nchi 'kuhamia Dodoma.' Tukio lenyewe si jipya, ni jambo linalotokea mara nne kila mwaka. Ni Kikao cha Bunge, ambacho hukutama mjini Dodoma kila Februari, Aprili, Juni na Novemba. Ujio wa kikao hicho katika mji wa Dodoma, katikati kwa Tanzania ni jambo la kujivunia kwa wakazi wa hapa. Kila kikao kibapokuja a tunawezakusema kila makao makuu yanapohamia Dodoma kwa muda, kila kitu huchangamka. Biashara hutembea kwa mwendo wa haraka, mzunguko wa fedha huongezeka na hakuna kisichopanda bei. Hata pombe ya choya ya weenyeji wa hapa hupanda bei. warembo wanaofanya biashara ya uzuri hupanda dau, nyamachoma ndo usiseme, gesti nazo hazishikiki bila kusahau taxi, ambapo zile za 'buku' sh 1000 huwezi kuzipata tena, mitumba ya tai nayo usiseme. Bidhaa inayobaki bei ile ile ni magazeti, lakini na yenyewe huletwa kwa wingi, ili kutosheleza mahitaji ya wakubwa waliosheheni mji wa Dodoma. Si hayo tu, hata 'serengeti boys' samahani namaanisha ombaomba, nao huongezeka mara dufu.
Maandalizi yote ya ujio wa makao makuu hapo Februari Mosi, 2005 ndo yameshika kasi na kwa makiso, mji utakuwa na wageni rasmi zaidi ya 400 kwa kipindi cha wiki mbili. Lakini yote kwa yote, matukio hayo ni ya muda tu. Wakubwa wanakuja kwa vikao na kuyoyoma zao kurejea Jiji la joto na maraha, Dar es salaam na kuacha suala la kuhamia Dodoma kama Makao Makuu ya serikali kuwa ndoto za alinacha. Tusidanganyane, hakauna kuhamia Dodoma. Byebye

1 comment:

Anonymous said...

Umeishia wapi?

Post a Comment