UONGOZI wa juu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo umepiga hodi nyumbani kwa Rais
Mstaafu, Benjamin Mkapa, Sea View jijini Dar es Salaam ili kupata maoni yake juu ya Katiba mpya.
Waliokwenda kwa Mkapa (wakiwa naye pichani) ni wajumbe wa Tume na Sekretarieti
ya Tume Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam wakiongozwa na
Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba (kushoto).
Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani (wapili kulia), Mjumbe wa Tume Dk Salim Ahmed
Salim (kulia) na
Katibu wa Tume Assaa Rashid (wa tatu kulia). Blog ya Kisima cha Fikra bado inaendelea kutafuta maoni yaliyotolewa na Mkapa, hata hivyo vyombo vya habari mbalimbali vimeshindwa kupata fununua ya alichosema, vikieleza tu kuwa ametoa maoni 'kimyakimya'.
No comments:
Post a Comment