Tuesday, January 15, 2013

Jimbo Katoliki Bukoba lapata askofu mpya



Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desderius Rwoma (kulia) akiwa na Askofu Nestory Timanywa anayestaafu uaskofu wa jimbo hilo baada ya kutimiza umri wa miaka 75 kwa mujibu wa sheria za kanisa. Kabla ya uteuzi/uhamisho, Rwoma alikuwa askofu wa Jimbo la Singida.

Wasifu


Askofu Desiderius Rwoma alizaliwa mwaka 1947 katika Parokia ya Rutabo, Kamachumu jimbo Katoliki la Bukoba. Parokia moja na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa.

Alipata upadrisho kwa mikono ya Askofu Timaywa, mwaka 1974 pale Rutabo.

·        Akiwa jimboni Bukoba aliwahi kuwa gambera (Mkuu wa shule) ya seminari ya Rubya kwa miaka mingi. Wakati wake shule ya Rubya mara kadhaa ilikuwa ya kwanza kitaifa katika mitihani na karibu mara zote ilikuwa kila mara kati ya shule 10 bora taifani. Mapadre wengi vijana jimboni Bukoba walipitia mikono yake hivyo anawajua vizuri na wanampenda.
·        Vile vile alikuwa mlezi wa kiroho wa shirika la masista wa Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu, shirika la jimbo na hivyo analifahamu vizuri na kila mara amekuwa  karibu nao.
·        Kabla ya kuteuliwa kuwa askofu wa Singida alikuwa makamu wa askofu na hivyo kulijua jimbbo la Bukoba na uongozi wake. Alifanya kazi hii vizuri sana na hivyo kuteuliwa kuwa askofu wa Singida.
·        Akiwa askofu wa Singida (1999 – 2013) ameonyesha karama zake za uongozi. Ameweza kuleta maendeleo ya kichungaji na kibinadamu katika jimbo. Ameonnyesha uelewano wake kwa kuwaalika mashirika mengi ya kitawa ambayo kila moja limeleta karama yake ya maendeleo, uchungaji, shule, vituo vya afya, maendeleo ya akina mama na vijana nk.
·        Katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anasimamia idara kubwa ya Utume wa walei
 Askofu Desiderius Rwoma akaelezwa na Askofu Msaidizi, Methodius Kilaini kupitia Mtandao wa Bukoba Group, kuwa ni mpole, mnyenyekevu, msikivu, muwazi na mpenda maendeleo. Ana uhusiano mzuri na kila mtu bila kujali hali, jinsia, kabila, taifa au dini.

No comments:

Post a Comment