Na Ndimara Tegambwage
LEO ni siku 172 tangu serikali ifungie gazeti la MwanaHALISI “kwa muda usiojulikana.” Siku hizo ni sawa na miezi mitano na siku 22 au miezi sita kasoro siku nane. Ni nusu mwaka.
Kwa muda usiojulikana maana yake ni mpaka serikali itakapotaka (yenyewe). Itakapojisikia. Itakapofurahi. Itakapopigiwa magoti na wamiliki wa gazeti. Itakapoombwa na marafiki wa gazeti. Itakaposhinikizwa vya kutosha na wapigania uhuru wa habari.
Kwa muda usiojulikana yaweza kuwa pale viongozi wa serikali waliofungia gazeti watakapotembelewa na akili na uelewa kuwa hawapaswi/hawakupaswa kuingilia uhuru wa kupata, kutafuta na kukusanya habari; au pale serikali itakapoamuliwa na mahakama; au wenye gazeti watakapoamua kulichapisha kwa mapenzi ya wananchi bila kujali serikali inasema nini. Hilo nalo linawezekana. Endelea nayo
No comments:
Post a Comment