Na Waandishi Wetu, Same
PAMOJA na polisi kusisitiza kuwa mtoto Grace Kelvin (5) aliyekuwa amepotea na wananchi kuchoma Kituo cha Polisi Hedaru hakuwa ametekwa, mtoto mwenyewe amezungumza na Majira na kueleza kuwa alichukuliwa na baba mmoja akamwambia anampeleka Dar es Dalaam kumnunulia soda na chakula.
Mtoto huyo ambaye anaongea kwa woga, alisema baba huyo alimwambia amuite baba, alipomuita baba, mtu huyo akamuuliza unakwenda wapi, yeye akamwambia yuko nyumbani kwao.
Baada ya jibu hilo, baba huyo alimuuliza kama amekula, naye akajibu hajala, ndipo mwanamume huyo alimwambia amfuate aende naye dar es Dar es Salaam ili ampe soda na chakula.
Alisema baada ya kumfuata alimpandisha kwenye daladala 'kwenda Dar' na walipofika alimuacha sehemu ambayo haijui lakini anadhani ndiyo Dar, baba huyo alimuachana mahali akamwambia anakwenda kununua vitu vya kupeleka nyumbani, hakurudi tena.
Baadaye alikuja mama mmoja akamuona amekaa muda mrefu, akamuuliza anafanya nini, naye akajibu alikuwa anamsubiri baba, baada ya kusubiri kwa muda mama huyo aliamua kumpeleka polisi.
Wakiwa polisi mtoto huyo alijitambulisha kama Grace Godfrey badala ya Kelvin, lakini baada ya kuandikisha polisi walimruhusu mama huyo kuondoka na mtoto huyo kwenda kulala nyumbani kwake.
Mtoto huyo alipatikana kirahisi baada ya kusambaa taarifa za wananchi kuchoma moto kituo cha polisi wakiamini kuwa ametekwa ili kutolewa kafara.
Mzama wa mtoto huyo, Bi. Glory Samwel alisema hakujua mapema taarifa za mtoto wake kupotea, na alikuja kupata taarifa za kupatikana kwake mjini Moshi.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi, Mkoani kilimanjaro, Lucas N'gomboko alisisitiza kuwa mtoto huyo hakutekwa bali alitelekezwa kwenye soko la Mbuyuni mjini Moshi.
Swali: Kama hakutekwa, alitokaje nyumbani kwao Hedaru, Same hadi Pasua mjini Moshi?
Je, Aliyemtelekeza alikuwa amemchukua kwa nia gani?
...mengine ongeza mwenyewe.
No comments:
Post a Comment