Thursday, November 25, 2004

Watatu waliwa na simba Dodoma

Nov 23

Na Reginald Simon, Dodoma

WATU watatu wameuwa na simba katika Kijiji cha Izava,
Tarafa ya Itiso Wilaya ya Dodoma Vijijini.

Tukio hilo lilitokea juzi (jumatatu) asubuhi baada ya
simba zaidi ya watatu kuwashambulia watu hao wakati
wakiwafuatilia ng’ombe wanne waliokuwa wamechukuliwa
na simba Jumapili saa 9 usiku.

Mmoja wa wanafamilia wa watu waliouawa, Augustino
Mwalimu, alilieleza gazeti hili kuwa, waliouawa
walikuwa miongoni mwa wanakijiji waliokuwa
wanafuatilia ngombe katika mlima wa Izava.

Alisema, mapema simba walivamia boma la mzee Masaka na
kuchukua ng’ombe wanne na baada ya tukio hilo
wanafamilia waliita wanakijiji wenzao na kuanza
kufuatilia hadi saa 5 mchana siku iliyofuata,
walipokuatana na simba hao na kuwazuru.

Waliouwa Jonathan Masaka (60 ambaye alivyofolewa koo,
Elias Suka (38), Jackson Chizoza (28) na mwanamke
Nthonyi Lebeleja (46) ambaye alikuwa na mtoto wa miezi
mitatu Elias Lubeleja aliyejeruhiwa vibaya na kulazwa
katika hospitali ya Izava.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, tukio hilo liliripotiwa
katika kituo cha polisi cha Dabalo na polisi
waliwasili katika eneo la tukio juzi saa 12 jioni na
baada ya kufanya uchunguzi waliruhusu miili ya
marehemu izikwe. Mazishi yalifanyika jana asubuhi.

Mwalimu alisema askari wa wanyamapori waliwasili
katika eneo hilo jana asubuhi na kuanza zoezi la
kuwasaka simba hao walawatu.

Tukio kama hilo liliwahi kutokea katika kijiji hicho
mwaka 1994 ambapo watu wa familia moja walishambuliwa
na simba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Wolfugang Gumbu,
aliliambia Mwananchi jana kuwa hakuwa na taarifa za
tukio hilo, lakini aliahidi kufuatilia kupitia kwa
Kamanda wa Polisi wilayani humo (OCD) na kutoa taarifa
baadaye.

Mwisho

No comments:

Post a Comment