Sunday, June 07, 2009

Askofu Akana Kushiriki Freemason

Askofu Jacob Koda (pichani mwenye msalaba, akiwa na mapadri walio chini yake) ambaye amevuliwa mamlaka ya kuongoza jimbo Katoliki la Same 'amezushiwa' kuwa hatua hiyo imechukuliwa kwa sababau anashiriki ibada za mashetani maarufu kama Freemason, lakini yeye ameibuka na kukana tuhuma hizo, huku akiweka wazi kile anachodai ni sababu ya hatua hiyo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti la Mwananchi, alisema: “Sijashiriki na sitashiriki dini hiyo lakini wanaozusha hayo mambo wajue muosha naye huoshwa, hivyo walivyonisingizia siku sio nyingi vitawarudi”.

Askofu Koda ambaye hata hivyo alisisitiza kuwa yeye bado ni askofu hadi milele kwa kuwa aliochoondolewa ni mamlaka ya kuongoza jimbo, alifafanua kuwa hatua hiyo dhidi yake inatokana na uchu wa madaraka, chuki binafsi na wivu wa maendeleo aliyoleta katika jimbo hilo.

2 comments:

Anonymous said...

namuona baba Mlacha hapo.

Anonymous said...

Wewe askofu mbona una maneno mengi? si utulie na kuendelea na upadri wako? mimi naamini wenzio sio wajinga kiasi cha kusikiliza majungu ili kukuondoa, lazima kuna jambo kubwa ulilofanya na wewe unajua hilo.
Tunajua kanisa katoliki halina desturi ya kutoa habari za watu kwa wazi zaidi, na hii mimi nafikili ni faida kwako, laiti kama yakisemwa yote itakuwa ni fedheha kubwa kwako na kanisa kwa ujumla.
Kuwa mtii baba askofu mbona mapadri mliowasimisha walikuwa watii na awakupiga kelele?
Una walakini tu kwa kuwa sijawai kuona mapadri waliosimamishwa upadre wakakimbilia kwenye vyombo vya habari. daima walikuwa kimya na wasikivu mpaka pale ukweli ulipojulikana.

Post a Comment