Thursday, February 05, 2009

Mtuhumiwa Muhimu


Mmoja wa watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa Mahenge, Rashid Lema ambaye ni mgonjwa kiasi cha kushindwa kupanda kizimbani akikokotwa kuondoka eneo la mahakama baada ya kesi yao kuahirishwa. lema ndiye aiyetoa maelezo ambayo walau yanazungumzia uhusika wa Zombe. Jana mawakili wanaowatetea washtakiwa hao, akiwamo aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe waliomba waachiwe kwa kukosekana ushahidi wa kuwatia hatiani, lakini leo, mawakili wa serikali walisema ushahidi upo wa kutosha na kuimba mahakama kuendelea na kesi yao ya mauaji. Mahakama inapitia hoja za pande mbili na uamuzi utatolewa Jumatatu.

No comments:

Post a Comment