Wednesday, February 18, 2009

Mchungaji na viungo vya albino

HII KALI

POLISI Mkoani Mbeya inawashikiliwa watu wawili wakazi wa Kijiji cha Idweli Kata ya Iyula Wilayani Mbozi, akiwemo mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Cosmas Mwasenga (39), kwa tuhuma za kupatikana na viungo vya albino ambavyo vilikuwa vikiuzwa kwa Sh 30 milioni.

Tukio hilo linalomhusisha mchungaji limekuja wakati nchi ikiwa katika kampeni kubwa ya kupambana na ukatili dhidi ya Albino, kampeni ambayo hupewa msukumo pia na viongozi wa dini mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Zelothe Stephen, alimtaja mtuhumiwa mwingine kuwa ni Luseshelo Mwashilindi (38) mkulima wilayani Mbozi. SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment