Wednesday, November 14, 2007

Mwanahalisi la leo: Linajieleza

Kama huwezi kusoma maelezo ya picha hii, imeandikwa hivi: "Kutoka Kushoto ni Kanali Jakaya Kikwete, Luteni Yusuf Makamba, Capteni George Mkuchika na Kapteni John Chiligati". Wote wapo katika vazi rasmi la kijeshi

2 comments:

Anonymous said...

Kama ni hivyo chama kinatisha kama nzige. Wapinzani watarajie mizinga tu

Anonymous said...

Kamaradi RSM,
Miaka ile ya Uongozi wa Baba wa Taifa na baadae Mzee Mwinyi tulikuwa na Mikoa 25 kijiografia lakini kichama na kiserikali tulikuwa na mikoa 26. Na Mkoa huo ulijulikana kama Mkoa wa Majeshi. Utawakuta akina Meja Jenerali Marwa wakiwania ujumbe wa NEC, na wanajeshi wengine wengi wakishikilia nyadhifa mbalimbali katika chama na serikali. Matokeo yake ndiyo haya mnayoyaona hivi sasa. Baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi, ilibidi dhana ya mkoawa majeshi ifutwe na wanajeshi wakapigwa marufuku kujihusisha na vyama vya siasa. Wengi wa wanajeshi waliokuwa na nafasi serikalini na katika ccm walijiuzuru uanajeshi na kujichimbia moja kwa moja katika siasa. Matunda ya kazi hiyo mnayaona leo. Luteni Kanali ndani ya suti akiingia Ikulu. Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Na hayo ndiyo mapinduzi. Kweli Mwalimu alikuwa anaona mbali.

Post a Comment