Friday, November 23, 2007

Hii Kali!...Eti Kabatilisha Kujiuzulu


Yule mnene wa lile lishirika lenye ukiritimba wa kuzalisha za kusambaza umeme pekee nchini Tanesco. Dokta Idrisa Rashid aliyetangazwa kwa mbwembwe jana na leo kuwa amejiuzulu mambo yake si mazuri. Si mazuri kwa sababu tunaweza kusema hana msimamo...au wakubwa zake wamemkatalia...au alikuwa anatishia nyau. Eti kabatilisha kujiuzulu. Mwananchi ilimwandika hivi. Mtanzania nao waliweka hivi. Sasa anaendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika linalokusanya mapesa kibao kutoka kwa kila aliyeunganishwa, lakini haliwezi kijiendesha...wala wakubwa zake kuamua kujizulu. Lazima wabaki ndani na maIPTL, Madowans, Marichmond, maSongas nakazalika...

No comments:

Post a Comment