Thursday, October 26, 2006

Nakataa, siwezi kukulamba miguu

Nilikuwa sijatoa msimamo wangu kuhusu 'kumlamba chifu miguu'. Binafsi, sikatai, najua wapo wengi wanaomlamba chifu wao miguu. Lakini mimi si miongoni mwao na katu sitakaa nimlambe chifu wangu miguu. Hata wale waliojitokeza kupinga, wanajua fika kuwa miongoni mwao wapo wanaolamba miguu ya chifu, lakini tatizo ni kwamba kikaragosi chenyewe kilichorwa na Mtz katika gazeti la jirani. (ukweli ungekuwa ukweli kama kingechorwa kwenye gazeti la Tz). Kwa vile najitokeza mara kwanza baada ya muda mrefu, sitaweza kufafanua zaidi ya hapo.

Hii ilikuwa ni kwa taarifa tu kuwa, pamoja na mambo mengi yanayonikabili, nitakuwa najitahidi kuendeleza mawasiliano kupitia blogu hii-RSM-

4 comments:

Anonymous said...

Kazi nzuri Reggy. Usilambe viatu. Watu wanaojizoeza lambalamba watajikuta siku moja wakilambishwa vitu vya ajabu!

Ukweli wa ambo haya hautatoka midomoni mwao. Utatka mioyoni mwao. Hata wakiongopa leo kuhusu hali halisi, itajulikana siku moja kwamba walikuwa wanajidanganya kwa kudhani wanatudanganya sisi.

Kinachonisikitisha ni kwamba kizazi kilizojiingiza kwenye lambalamba hii ni kile ambacho kngeandaliwa kubuni, kujenga, kuimarisha na kulinda misingi.

Ni kile kile ambacho kingepiga vita corruption. Sasa nacho kimekubali kuingia katika corruption. Kimeikumbatia! Kinaitetea na kuishangilia.

TUnahitaji manabii kumwaga OLE kwa kizazi hiki? Hapana. Hebu tukisaidie kabla hakijalaaniwa. Tukiambie. Kitasikia. Hata kisipokubali, kitakuwa kimesikia.

Wahaya wana usemi kwamba NYANI ALIKALIA JIWE HALAFU AKATO USHUZI UNANUKA VIBAYA. AKASUBIRI KUONA KANA JIWE LINGELALAMIKA. WAPI! AKALIGEUKIA NA KULIAMBIA: "HATA KAMA HUJITINGISHI, UMEIPATA!"

Tumeshafikana hapo. Tumeashakata tamaa kwamba hawa hawasikii? Au tumesema kidogo? Tuwaache wahukumiwe baadaye kwa matendo yao? Tuwaamshe lakini tusilale pia? Leteni hoja.

Rashid Mkwinda said...

Hii sasa kali ya kuramba viatu mie simo jamaa naona ameamua kujitosa unajua wenzetu Wakenya tofauti na siye huku lakini hata hivyo mie nadhani ujumbe umefika kama ni kweli siye twawalamba viatu machifu wetu ama la, cha muhimu hpa nadhani waandishi tunatakiwa kubadilika tusiwe tegemezi na hatimaye tukatumika kama vinoo vya kunolea visu ili vikakate nyama kwingine maana tumetumika sana wakati wa kampeni za kisiasa na hatimaye baadaye tukaanza kutukanwa na baadhi ya wabunge.

Tubadilike tusiwe tegemezi hatuwezi kutukanwa na kusemwa kwamba tunaramba viatu vya machifu wetu lakini kuna ukweli fulani kutokana na mazingira ya waandishi wa Tanzania hatuna vitendea kazi tunategemea kudandia magari ya wabunge, mawaziri na ndege za viongozi, ndio maana hawa wenzetu Wakenya wanatutukana namna hii tubadilike,,TUBADILIKE

Anonymous said...

Kamaradi RSM, Msimamo yako usioyumbisha ima kutikiswa naufahamu sawia. Nakupongeza sana kwa kukataa kulamba viatu. Na wala usithubutu kufunga kamba za viatu hivyo au kuvisogeza kwa mwenye avivae huo utakuwa ni UTUMWA. Utumwa hudhalilisha na kuvunja heshima. Utumwa ufunga kauli na akili. Huwezi kuhoji achilia mbali kukemea. Katu usiikubali "Hewala". Hewala si utumwa? Kweli?! Hewala ni utumwa. Ukikubali kulamba viatu leo, kesho je?
Nakupongeza sana kwa kuulinda uhuru na heshima yako na juu hayo kuilinda hadhi ya taaluma ya uandishi.
Karadi Amani

Anonymous said...

Bwana mkwinda ulosema ni kweli. Lakini kwa taarifa tu, ni kwamba hilo jiwe la kunolea visu ili vikate kwingine, hatimaye nalo humong'onyoka taratibu na kumalizika. Hii inamaanisha kuwa hata wale waandishi wanaotumika kama dodoki, ipo siku 'watakwisha'. Mtu anachuja, anaandika wasomaji hawasomi, hata waliomtumia wanakosa imani naye, kwa kudhani kuwa anatumiwa na wengine, kwa kuwa ndiyo tabia yake.Alamsiki

Post a Comment