Friday, April 07, 2006

Breaking News! Msaki Huyu Hapa

Ahadi ni deni. Leo nimelipa deni langu na kuwaletea picha niliyoahidi ya wanablogu waliokutana Dodoma, akiwemo almaarufu Mzee wa Kurunzi, Mark Msaki (wa pili kushoto), akifuatiwa Martha Beatrice Mtangoo na Hudson Kazonta. Kushoto ni mimi Reginald Miruko (RSM). Hapa tunatakiana maisha marefu baada ya kikao chetu kilichopitisha maamuzi mazito ambayo nitayachapisha baadaye.

8 comments:

mwandani said...

shukrani, tumewaona, mara moja moja tudondoshe picha nzima nzima.

Rama Msangi said...

Siku ya leo imekuwa nzuri sana kwangu maana nimeongea kwa undani sana na watu wawili muhimu sana katika Ulimwengu wa Blogi ambao ni Mark Msaki, ambaye alikuwa mjini Dodoma wakati naongea naye na ndugu yetu wa vijimambo, MK, ambaye alinitwangia akiwa London.

Nitazungumza mengi kuhusu tuliyoongea baadae, ila kwa sasa nimekaa mkao wa kusikia maazimio ya mkutano wa baadhi ya wana-Blogi wa Kitanzania uliofanyika mjini Dodoma (nadhani ilikuwa katika ofisi zaaaaaa.........)

boniphace said...

Kama na mimi nipo vile, hapa nashusha tabasamu kidogo na kisha nacheka naona wamiliki wenzangu wa magazeti Tando wanakutana. Huku kwetu tunajenga jumuiya na sio upinzani wa kibiashara kama ule wa akina Mengi na Shigongo. Safi sana, meshimiwa Mark, safi sana tunangoja agenda mlizojadili kisha kuanza mwongozi wa safari yetu ndefu. Asante sana Miruko

Jeff Msangi said...

Inatia hamasa sana kuona jumuia hii inakua namna hii.Anayedhani jumuia hii ni utani nadhani anafanya kosa la jinai na wala hana habari na historia zote za mapinduzi popote pale duniani.Tunayasubiri mliyoafikiana kwa hamu ili tuzidi kusukuma mbele jumuia hii.Naona mliheshimu ofisi na kuagiza coca badala ya zile "juice za maembe" za Mwaipopo na Makene.Kila la kheri hapo makao makuu ya kusadikika.

John Mwaipopo said...

Naandika maoni haya kabla sijasoma maoni ya wengine hapo juu. Kumbe blog si serikali tosha tu. Yaani mmekutana hivi-hivi. Linalonifurahisha kuwa undugu unajengeka miongoni mwetu. Boniphace Makene alipokwenda Canada alipokelewa na kutembezwa Toronto (kama sijakosea jiji) na Msangi Mkubwa. Kumbe hata nikienda Arusha naweza kupokelewa na wanablog huko. Kadhalika nikienda "duniani" aliko Ndesanjo. Keep up the Spirit! Kadhalika nikirejea Mbeya Mkwinda, Msangi mdogo na Nyembo tunaunda kaserikali ketu.

Mark Msaki kumbe kipande ya mtu (Mkwinda umeona faida ya kitimoto).

Mija Shija Sayi said...

Kwanza niungane na Mwaipopo.."Mark Msaki kumbe kipande ya mtu"...
Inatia raha sana na ninaamini iko siku tutakutana wote.

Martha Mtangoo naomba kukuuliza yule mwanamke wa kwanza kufungua blogu ya kiswahili ameenda wapi siku hizi? maana naona hata kwenye kikao hicho hakuwepo. Hebu fanya kumsaka na kumrudisha, tumemkosa mno.

mzee wa mshitu said...

Inafurahisha sana uhusiano kujengeka kwa kiasi hiki kumbe ni kitu kizito siyo mzaha. Halafu naona hapa Reginald akitafuna Coca Cola na washikaji wote itabidi hawa Coca Cola wawalipe fedha nyingi sana sababu mnaendelea kuwatangaza mpaka kwa kina mpaka Canada,kwa kina Msangi, Marekani kwa kina Ndesanjo, makene, mwaipopo na wengine kibao. Japo wanajulikana kote huko

Big Up Mark Msaki kumbe uko bonge ya jitu namna hiyo hii inafurahisa sana tunasubiri maamuzi ya kikao chenu hicho nadhani unaweza kuwa ni mwongozo madhubuti. Reginald Big Up naona mambo siyo mabaya gazeti naona linazidi kuboreka siku hadi siku hadi litabadilika na kuwa mtandao keep it up!

Martha Mtangoo said...

Da Mija ni hivi yule mwanamke wa kwanza kufungua Blog yupo lakini nafikiri siku hizo ana majukumu mengi sana kupita uwezo sasa itabidi Nimkumbushe tu kuweka vitu vipya mara kwa mara, usijali ataonekana tu!! na kaka rama hizi ni Ofisi za Mwananchi Communication Ltd (MCL), Jijini Dodoma.

Post a Comment