Tuesday, December 07, 2004

Karaha za likizo: Niende au niache?

Ya tatu ni TRENI. It’s demanding in terms of time. Haina uhakika wa kufika kwa muda uliojipangia na mbaya zaidi unaweza kufika Mwanza ukakuta meli imeshakuacha, ukalazimika kubaki katika Jiji hilo la mawe na barabara mbovu (sorry, of new tarmac road network) kwa siku zaidi ya tatu bila kutarajia.

Katika njia hii iliyojengwa na Mdachi, kuna wimbi la biashara ya vyuma chakavu inayochochea wizi wa mataluma ya reli, nati, na boliti zake. Sitasema matokeo ya wizi huo endapo hilo litatokea wakati huu.

Siwezi kusahau urushaji wa tiketi katika stesheni za treni. Mfano mzuri ni huu; Desemba 3 nilikwenda ‘kubook’ tiketi ya Desemba 7. Majibu ya mkatishaji wa tiketi yalikuwa hivi: “Hatuna nafasi hadi Desemba 25” Yaani siku ya xmasi.

Siku mbili zilizofuata nilimtumia mtu anayefahamiana naye, akapewa tiketi hiyo mbele yangu ikisindikizwa na maneno, “Lakini nimekupa ya mwanafunzi.” Dalili za rushwa!!!!! Pamoja na Matatizo yote haya, nimechangua usafiri huu wa treni.

Mpenzi mgeni wa siste hii ya RSM, ni dhahiri kuwa utamiss mambo mapya nitakapokuwa likizo. Haitakuwa rahisi kukupatia mambo, kwani kijijini kwangu, kama ilivyo maeneo mengi ya TZ, hakuna umeme na hivyo kompyuta ni ‘mashokolo mageni’(jambo lisilofahamia).

Nikiwa huko sitaweza kupata comments zao, sitaweza kukuandikia. Na hoja kwamba dunia sasa ni kijiji haitakuwa na maana. Bye

No comments:

Post a Comment