Naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema ana sababu za msingi za kuamua kuuwania uenyekiti wa chama hicho, huku mwenyekiti wake Freeman Mbowe akimkaribisha katika kinyang'anyiro hicho.
Tumefukuza sana wanachama. Haiwezekani tukajenga chama cha kufukuzana tu. Ni lazima tukubali kutokubaliana," alisema.
"Kugombea kwangu ni wito wa kurejesha umoja katika chama wakati tunajiandaa kuchukua dola. Uchaguzi Mkuu wa 2010 utakuwa wa kihistoria kwa kuwa kwa uzoefu wangu unaweza kulazimisha serikali kuundwa na waziri mkuu ambaye hatoki CCM. Hatuwezi kwenda huko tukiwa divided (tumegawanyika)." Soma kwa kina
No comments:
Post a Comment