Thursday, May 21, 2009

Pole Sana Mwakyembe








Nampa pole Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe aliyepata ajali leo asubuhi mkoani Iringa karibu na eneo la Mafinga akiwa njiani akitoka Kyela kuelekea jijini Dar es Salaam. Walioshuhudia tukio hilo wanaeleza kuwa gari la Dk Mwakyembe lilipata ajali baada ya kukwepa lori na kisha kutumbukia katika korongo ambapo tairi lilichomoka gari limeharibiwa vibaya na Dk Mwakyembe mwenyewe amekimbizwa hospitalini mkoani humo, na taarifa za karibuni kabisa zinasema kuwa Bunge limetoa ndege na kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Habari kamili Ziko Hapa-RSM-

1 comment:

Anonymous said...

Pole sana Mpendwa katika kristo

Post a Comment