Habari ndiyo Hii
ALIYEKUWA Hakimu wa mahakama ya wilaya Temeke, Jamila Nzota amehukumiwa kifungo cha miaka miaka 11 jela, lakini atatumikia mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh 700,000.
Hukumu hiyo ilitolewa leo na Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumwona ana hatia kutokana na mashahidi tisa waliotoa ushahidi katika kesi hiyo.
Nzota alihukumiwa miaka 11 kwa mashtaka manne yaliyokuwa yanamkabili, lakini atatumikia adhabu zote kwa pamoja kwa kifungo cha miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment