Monday, May 25, 2009

Matokeo ya awali Busanda


Kura ya maoni iliyopigwa na wasomaji wa blog hii, Kisima cha Fikra, imeonyesha kuwa Chadema imeibuka mshindi huko Budanda kwa asilimia 78, CCM inafuatia ikiwa na 18%. CUF na UDP wanalingana wakiwa na asilimia tatu (3%) kila chama (angalia hapo kulia kwenye poll) .

Lakini uhalisia wa mambo huko Busanda ni kinyume kabisa, kwani hadi asubihi leo CCM ilikuwa inaongoza ikiwa na kura zaidi ya 29, 000; Chadema zaidi ya 21,000 CUF 900 na UDP 380. Taarifa kamili zitakuwa hapa kadri matokeo yatakavyotangazwa.

1 comment:

Anonymous said...

Kaka habari
Mimi nimekua mfuasi wako kabla na baada ya kutangaza ungeacha kublog na mimi nilikua mmoja wa watu niliokutumia ujumbe nikikutaka uendelee kutupatia habari maana ulimwengu wa sasa tunahitaji habari kutoka kila sehem na maada mbalimbali

Vilevile mimi nilikua shabiki wa Marehem Kabuye na hakuna siku niliyofurahi kama niliposoma interview yake uliyofanya naye

Kwa kifupi na mimi nimeingia kwenye kublog na nilikua naomba tu kushirikiana na wewe japo mimi ninalengo la kua natoa habari mbalimbali katika sports and entertainment industry anuani ya blog yangu ni; http://godnyam.blogspot.com/

Nakushukuru sana na naomba unisaidie kwa lolote litalonifaa maana najua wewe ni nguli katika uandishi wa Habari

Asante sana naitwa Godfrey

Post a Comment