Mishale hii ya saa 9 mchana, yale mabomu yaliyosalia kwenye ghala la silaha huko Mbagala yanaaza kufyatuli kwa lengo la kuharibiwa kwa kuwa inaelezwa ni hatari zaidi kuyatunza (yalishapata mtikisiko). Pia ni hatari zaidi kuyahamisha mahali hapo. Zoezi hilo litaenda hadi mishale ya saa 11 jioni. Wananchi wamepewa tahadhari ya kukaa umbali wa mita 500 kutoka kambi hiyo ya Kizuiani, lakini imeelezwa kuwa hayatakuwa na athali kama yale ya mwanzo. Maelezo zaidi-RSM-
1 comment:
Watanzania tuna tabia moja ya ajabu. Kukitokea tukio la kutisha, kama vile ajali, tunakimbilia kwenye tukio kwenda kushangaa.
Hata haya mabomu yalivyolipuka Mbagala, tulipata taarifa kuhusu Watanzania walivyokuwa wanakimbilia huko, na ikabidi askari wafanye kazi kubwa ya kuwafukuza.
Sijui ni nini kinachotufanya tuwe hivyo, lakini baada ya tukio, kila mtu anataka kusikia stori zinavyovuma huko vijiweni, kwenye baa na dala dala. Na Watanzania kwa kusimulia stori, pamoja na kutia chumvi, hatujambo.
Post a Comment