Saturday, March 07, 2009

Zitto aibuka, alonga

Msimamo wa Zitto

I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country.

I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.

Nimetukanwa sana humu. Nimesimangwa sana humu na kuzushiwa kila aina ya tuhuma. Ninajijua kuwa sina bei. Siwezi kununuliwa na yeyote. Ninajijua na nimekuzwa kusimamia yale ninayoamini hata nikibaki peke yangu. Siyumbi. Siyumbishwi. Niliokuwa nao Chuo Kikuu wanajua nilivyo.

Nimefuatilia sana mjadala huu na kuona umejaa hisia kali sana. Ninajua ni hisia za watu wanaopenda nchi yao. Ninajua ni hisia za kizalendo. Sina mashaka na hili hata kidogo. Hata hivyo uongozi hauendeshwi kwa hisia tu. Uongozi wa nchi ni zaidi ya hisia na maneno matupu (hot air).

Nimesema hapo awali kuwa kwa kuwa Watanzania wamezoea kuwa na viongozi wala rushwa na waongo, itawachukua muda kukubali viongozi honest. Hata hivyo, muda huo utafika tu.

Hata hivyo, ni vema sana tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu wengine. Kwamba leo mtu akiamua usivyotaka kanunuliwa? Je hayo maamuzi mengine hayawezi pia ya kununuliwa? Hapana, nadhani pale ambapo mwingine ana maamuzi tofauti ni vema kuheshimu maamuzi hayo bila kumwita kila aina ya majina mabaya.

Mimi binafsi, ninaamini kabisa kuwa hoja za TANESCO kuhusiana na suala la equipments hizi ni hoja zenye mshiko. Hoja za Kamati ya Nishati na Madini ni hisia za kisiasa. Sio kweli kuwa TANESCO hawakuja katika kamati na alternatives. Walikuja na alternatives kadhaa na zote tulizijadili.

1. Walieleza kushindwa kwa Kiwira kuzalisha 50MW mwezi huu na pia 150MW mwezi wa Septemba.

2. Walieleza mradi wa Kinyerezi wa 240MW kushindwa kuanza kupitia PPP kufuatia wawekezaji kukosekana

3. Walieleza mradi wa umeme wa upepo Singida kukwama

4. Walieleza kuhusu mradi wa 300MW wa Mtwara.

Katika hili mnawalaumu TANESCO bure tu. walitoa altrnative ya Dowans. walisema mbadala ni kununua mtambo mpya lakini walitahadharisha muda kwani mitambo mipya haipo tayari imetengenezwa na kuwekwa katika show room. Huwa inakuwa ordered kwa mtengenezaji na kuundiwa, kisha kufungwa na baadae kuwa commissioned ndio uanze kazi.

Mwanakijiji alizungumzia umeme wa Zambia. Tunanunua umeme wa Zambia na ndio unatumika Sumbawanga. Umeme huu ni mdogo sana na ubora wake pia ni mdogo. Kimsingi nchi zote za SADC zina tatizo kubwa sana la Umeme isipokuwa (potentialities) Msumbiji, Tanzania na Congo DR. Mwanakijiji alizungumzia Stigler's gorge. Huu ni mkakati wa muda mrefu. It takes time kujenga hydro plant.

Kule Kigoma wanajenga Malagarasi mini hydro, itachukua miaka 2 (8MW). Ni rahisi sana kuzungumza masuala haya lakini realities are different. Ninashauri baada ya mjadala huu wa TANESCO na DOWANS kuwa umekwisha (TANESCO wameumaliza) tuanze mjadala sober kuhusu 'energy sector' in Tanzania. Tuwe proactive na sio reactioneries. Power masterplan ipo.
Haitekelezeki. Energy policy ipo. Tujadiliane baada ya kadhia hii ili tuone nchi yetu iendaje katika sekta ya Nishati. Source: Bidii@googlegroups.com

Hapa akajibiwa

On 3/7/09, Monica Malle < moninaike@hotmail.com > wrote:
Mh. Zitto unayosema hayaingii akilini kwa mtu yeyote kwani udharura wa umeme mbona tunao siku zote kila siku umeme unakatika mara tunaambiwa hili mara lile mara mgao wa wiki moja hii ni dalili kuwa hata hiyo mitambo ya Dowans haifanyi kazi. Kama umeshapewa cha juu heri unyamaze kuliko kujifanya eti hununuliwi ,hela ilimnunua hata Yesu itakuwe wewe Zitto tunayekujua? ndumila kuwili Kwani Tanzania bila Dowans umeme utakuwa haupo?
Kwanini turudie matapishi yetu tuliyotapika? (Richmond)? Kwanini tuvunje sheri ya manunuzi kwa ajili tuu watu wa aina ya kina Zitto wanataka kumegewa asilimia 10? Kama wanaikumbatia hiyo Dowans basi akina Lowasa waruduishwe madarakani , waliwajibishwa kwa sababu gani? Nao viongozi wa Tanesco na waziri Nishati wasitutishe waanze kuachia ngazi kabla hatujaitisha maandamano nchi zima kuwalaani kama mafisadi.
Pia watangaze tenda ya kununua mitambo mipya haraka iwezekanavyo wasitutishe siku tukiwa gizani tutajiu? watajiju wao, kwani inapita wiki bila kuwa gizani? hilo tumezoea tunataka watu creative sasa sio wanaoshi kwa kusubiri Ten Percent. Nawe raisi sema chochote tujue msimamo wako sio unangoja mambo yakisha kuwa mabaya unajitokeza kwenye Tv na tabasamu.
TWATAKA MITAMBO MIPYA HARAKA IWEZEKANAVYO. HIYO YA DOWANS KAMA ZITTO ANAITAKA AKAIFUNGE JIMBONI KWAKE HUKO KIGOMA KASKAZINI HAWANA UMEME.

Zitto akahitimisha

Monica,Unanishambulia bila sababu.
Mimi sio Ndumilakuwili. Ninaweza kuwa nina unpopular stand lakini hiyo haifanyi kuitwa ndumilakuwili. Nimesema nipo tayari kuwa held accountable kwa msimamo wangu huu ambao haukubaliwi na watu wengi. Ndio price of leadership. Nipo tayari kuilipa. Siwezi kupima upepo wa kisiasa na kugeuka. Hapana.

Mpaka sasa ninaamini kuwa maelezo ya TANESCO kwenye kamati yangu yalikuwa in good faith na mahitaji ya umeme nchini ni real. Growth of the economy requires more energy and our capacity to produce it is limited. And i know the economic consequences of load shedding.

Review our economic statistics of 2006 and you can not comprehend. I said it once that, a circuit breaker at Kidatu broke and we had load shedding in January. Reason: We did not invest in TANESCO for the last 10 years due to privatisation process. TANESCO was specified company till 2007. The much despised Dr. Idriss Rashid took over TANESCO in 2007 and cleaned it from a disclaimer audit opinion to an unqulified one.

Now he tells us, we have deficit and one of the option (short term) are the used Dowans turbines, we say all the words. Thabit Kombo once said - tuweke akiba!Patriotism, truth and trustworthy are principles of my life. I was raised so and i live so.

1 comment:

stey said...

Mkubwa sikuungi mkono hata kidogo.Pamoja na mechanism unayojaribu kuielezea lakini , hapo bado haingii akilini hata kidogo.Hii ni betreyal.Mtanzania mkweli kesha kufa, at your age tulitegemea tofauti kubwa katika mwenendo mzima wa siasa za kifisadi zinazo tuumiza .But seems no changes.

Post a Comment