Jana, Mei 31 ilikuwa siku ya kutotumia tumbaku duniani. Nani anakubalina maudhui ya siku hii?. Bila shaka ni wachache. Wakati Tanzania inategemea sana tumbaku katika mapato yake, na Kampuni ya Sigara (TCC) ikiwa ya pili kwa kuingiza kodi kubwa baada Kampuni ya Bia (TBL), makampuni ya tumbaku yanazidi kuimarika na kuongeza wavutaji nchini na duniani kwa ujumla. Tazama hapa. Inafahamika duniani kote kwamba matumizi ya tumbaku ni hatari, husababisha kansa na magonjwa mengine.
Watu mbalimbali mashuhuri wana maneno juu uwezekano wa kuzuia tumbaku. Soma misimamo yao hapa. Inatia moyo kuwa walau kuwa Tanzania imeshatunga sheria hii (makala ya Rose Haji)ya kuzuia matumizi ya tumbaku katika kadamnasi,ingawa utekelezaji wake haujaonekana. Tunataka kuona vitendo.
Taarifa za karibuni zinasema vijana wanavutiwa zaidi na tumbaku. Hali hii inachangiwa na mabango mazuri ya matangazo ya sigara, yanayohusisha vijana, sigara na hali bora za maisha. Usishangae kuona hata watoto wa kike nao wameanza kuvuta kama Makala hii ya Sharon Sauwa inavyoeleza. Tunachotakiwa kuvalia njuga sote ni kuzuia kabisa uvutaji wa tumbaku kwa kueleza kwa undani hathali zake. Soma hapa uelewe zaidi.
Hata hivyo, ulevi si wa tumbaku pekee yake. Hata pombe kwa sasa ni tatizo kubwa nchini. Irene Kakiziba Bwire wa TAMWA amenitumia makala hii fupi, akizungumzia matatizo ya ulevi wa pombe kwa wanaume (men) labda kama ametumia men kumaanisha jinsia zote. Hali inakuwaje kwa wanawake (women), isome hapa uone pia matatizo yake. (TAMWA ni Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, wanaopigania usawa wa kijinsia)-RSM-
No comments:
Post a Comment