Uchaguzi wa Mitaa nani Mkweli?
BILA shaka msomaji umesikia mengi kuhusiana na uchaguzi wa vitongoji uliofanyika nchini kote Jumapili Nov 21.
Matokeo yameanza kutangazwa nchi nzima. Lakini cha kushangaza ni jinsi vyama vya siasa vinavyojitangazia ushindi, na vingine kukanusha. Hapa kuna masuala kadhaa yanayofaa kuingizwa kwenye kona ya 'hoja mahususi' wiki hii:
Mosi, Wanaotangazia ushindi wanajua kwamba si jukumu lao kufanya hivyo.
Pili, wanaotangaza matokeo hayo nao wanajua kwamba wanaotoa taarifa hizo si wahusika rasmi na zaidi wote wana lengo la kujifagilia.
Tatu, wanaohusika na kutoa taarifa zilizo sahihi bado wamekaa kimya, kwa nini? huenda wanatumiwa au ndo mchezo mchafu umeanza.
Kwa mantiki hizo, sioni sababu ya viongozi waliopewa dhamana ya kutoa taarifa kuhusina na uchaguzi huo kukaa kimya wakati watu wasiohusika kutoka vyama vyote wakijitangazia ufalme hewa.
Kutokana na hayo, naona ni budi kila mhusika achukue nafasi yake sasa na katika uchaguzi wa VIJIJI na MITAA hapo Jumapili, Novemba 28
1 comment:
Post a Comment