Saturday, May 23, 2009

Kibano cha Mengi Kuumiza Wengi

Idara ya habari inaandaa mabadiliko ya Sera ya Habari. Sera inapendekeza kikomo cha umiliki wa vyombo vya habari. Ukimiliki kituo cha kurusha matangazo ya radio, basi ni radio tu, kama ni TV basi ni TV tu, kama ni magazeti basi ni magazeti tu. Sera hii ambayo itafuatiwa na sheria itamtaka mtu yeyote anayemiliki vyombo vyote vya habari, kama vile Reginald Mengi, kuamua kuachia vyombo vingine ili abakie na kimoja tu! Atapewa muda usiozidi miaka mitano kuwa ametekeleza sera/sheria hiyo kikamilifu. Bila shaka kibano hiki kwa sasa ni dhidi ya Mengi, lakini bila shaka watakaoumia hapo baadaye ni wengi. Source: Jambo ForumNo comments:

Post a Comment