Sunday, November 18, 2007

Zitto Kabwe Aibuka

Kabwe akiwahutubia wanafunzi wa elimu ya Juu jijini Dar es Salaa Jumamosi
Baada ya kumaliza kifungo chake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameibuka na kueleza kuwa kifungo hicho cha miezi mitatu nje ya bunge, hakijathubutu kubadili msimamo wake. "Zitto ni yule yule...Bado niko Vile vile" alieleza jana. Soma Hapa...JK Naye kamteua kwenye kamati ya kuchunguza mikataba ya madini. BUnge lilimkataalia kuunda kamati kama hiyo. Tusio na macho tunaona kuwa ameula, lakini wenye macho wanaona mbali zaidi kuwa JK kafanya hivyo kummaliza kisiasa...Itawezekana kamati nzima ibaini mambo, Zitto peke yake awe na msimamo tofauti?...tungoje kamati imalize kazi zake, kisha ili tuone kama itawezesha mikataba mibovu ambayo imeshasainiwa itabadilishwa au yatakuwa yale yale ya IPTL na City water...Kalaghabao

1 comment:

Anonymous said...

Kamaradi nafurahi uko tena kwenye ulingo.

Post a Comment