Wednesday, May 04, 2005

Ni Kikwete, wengine wajinyonge

YAMETIMIA. Moshi mweupe ulionekana jana katika Ukumbi waChimwaga baada ya 'Makardinali' wa CCM kuchinja majinamawili ya mwisho na kutoa moja 'takatifu'.
Waliochinjwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Tawala, CCM, jana ni Waziri Mkuu, Frederick Sumaye na waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, Dk. Abdallah Kigoda.
Baada ya hatua hiyo, walibaki Profesa Mark Mwandosya, Dk. salim Ahmed Salim na Bw. Jakaya Mrisho Kikwete, waliopelekwa katika Mkutano Mkuu, Chimwaga, Dodoma, Tanzania.
Baada ya Kuchekecha, Jina la Kikwete lilitoka na ushindi wa kishindo wa 64.2%. Alipata kura 1,072, Salim 476 na Mwandosya 122. Uchaguzi haukurudiwa na kura 4 ziliharibika. Kati ya hizo, moja haikuwa na jina lolote (blank) na tatu zilikuwa na majina zaidi ya moja. Kikwete, mbali na kupigiwa debe kinamna na Rais Benjamin Mkapa katika dokezo la Mwenyekiti, jina lake lilikuwa linatarajiwa na wengi, Soma Aman Milanga aliyeko Uingereza anavyosema.

No comments:

Post a Comment