Baada ya kuona kinyang'anyiro cha urais kupitia Chama Tawala (CCM) ni kikali, nilifikiria kuchukua fomu kupitias upinzani. lakini baadhi ya marafiki zangu niliowaomba ushauri, wamekataa katakata.
Mmoja wao, Albert, aliandika hivi:
Sitaki, nasema sitaki kusikia. Kamwe wala siwezi kukuchangia pesa ya kuchukulia fomu Chadema. Hata wengine wakikuchangia na ukapita, kura yangu hupati kwasababu huna hata sifa moja ya kuwa kiongozi wa nchi yetu. Kwanza wewe sio maarufu, hupitii chama tawala, huna kitambi, sio muongo, huwezi kuwa mnafiki na kwa kieleele chako ukaamua kwenda kuishi Dodoma, wakati "makao makuu" ya nchi yako jijini Dar, wanakoishi wenye sifa za kuiongoza Tanzania. sifa nyingine zinazoku disqualify ni upeo wako mkubwa wa kuelewa mambo na dunia inavyokwenda, unapenda utawala wa sheria, heshima kwa katiba ya nchi na uwajibikaji kwa wananchi wenzako. kwakweli huna sifa na kamwe hufai kuiongoza nchi yetu kwani itakwenda kuzimu. Waachie wenye sifa watawale ebo.
Naye Amani, akaongeza: "Hakika una hoja. lakini katiba inakuwa kikwazo. Umri. Au utakuwa Kihiyo. Au Diallo. Wao degree zinapungua kila uchunguzi. Weye umri utaruka kila mwezi. Oktoba utakuwa 40!
Naandika cheki sasa hivi. Hiyo nitatoa yote. Ingia katika chama twawala kisha chukua chako mapemaaaaa".
KWA UJUMLA Maoni haya ya marafiki zangu wanaosoma blogu hii, ni kwamba, kwa mazingira ya Tanzania, yaliyojengwa na CCM, si rahisi kabisa mtu aiyekuwa mwanachama wa CCM na zaidi asiyekuwa "mwenzetu" hawezi kupata urais. Pia vijana wasahau kuwa marais wa nchi hii hadi wazee wote watosheke. Itakumbukwa kuwa wanaojiita vijana sasa, wana umri wa miaka 55 na zaidi.
No comments:
Post a Comment