"Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber."-Plato
Wednesday, January 12, 2005
Sherehe za kukaribisha mwaka hadi Desemba!!
Ni maajabu, lakini hayastajaabishi sana. Kila mtu kwa uwezo wake kifedha, samahani kwa fedha za wakeshahoi zilizoidhinishwa katika bajeti ya Mheshimiwa sana Basil Pesambili Mramba anaendelea kutumia fedha za walalahoi kwa kula nyamachoma, kunywa deengelua na kusaza makombo ili 'serengeti boys' yaani ombaomba waje kuchukua, eti anakaribisha mwaka mpya. Kwani usipoukaribisha hautakuja! Alianza Omari Mahita, IGP wa maafande. Walau yeye aliwahi alikaribisha mwaka katika mkesha ule ule; Na fataki zinazozuiliwa na polisi zilifyatuliwa kwa wingi. Siku iliyofuata, akafuata Mkuu wa serikali, PM, Sumaye naye akaweka mbwembwe zake. Moto uliowashwa Januari Mosi ukaendelea kusambaa hadi huko kwetu mabonde kwinama, Dodoma, ambapo mkuu wa kaya Mzee Nkhangaa ameshaitisha party yake hapo kwenye ukumbi wa bunge. Kana kwamba haityoshi, sherehe zimeendelea kupamba moto na kuvuka siku ya 10 ya mwaka mpya, sorry, mwaka 'Mkuu kuu' uliochakaa wa 2005. Jana tu, imefanyika party kubwaaaa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma. Nadhani sasa tuendelee kusubiri shere za wakuu wa wilaya, makatibu tarafa, makatibu kata na hadi kufika ngazi ya vijiji, mwaka mpya utakuwa unaendelea kuadhim,ishwa hadi Desemba.
No comments:
Post a Comment