Tuesday, January 04, 2005

Nimekwenda, Nimerudi

# Safari Balaa

Kama nilivyokuelezeni wakati nakwenda likizo, kuwa nina wasiwasi na safari ya kutoka Dodoma hadi mikoa ya Kanda ya Ziwa, ndivyo hali ilivyokuwa.

Kila aina ya usafiri niliopaswa kutumia ulikuwa wa shida. Treni haikuwa rahisi kupata tiketi kwa sababu wasafiri ni wengi na watumishi wa TRC wanasingizia ni nyakati za wanafunzi ili wapate "mkono wa heri".

Lakini pamoja na yote nilisafiri kwa treni na kurudi kwa treni lakini kwa kuongeza kitu kidogo katika nauli ya kawaida.

Mabadi nayo utekeji ulikuwa umeshaanza. Siku chache baada ya mimi kuwasili mkoani Kagera, nilisikia katika vyombo vya habari kuwa badi la Bukoba limetekwa na abiria kuporwa mali na fedha. Jingine wakati narudi lilipata ajali na safari kukwama.

Ndege, hiyo siwezi kuijadili kwa kuwa uwezo wangu ni ule ule mdogo. Kwa lugha laini siiwezi.

tuendelee kushauriana, hadi barabara ya kati itakapokamilika kwa kiwango cha lami.
alamsiki

1 comment:

Anonymous said...

Ndio Reginald, karibu sana kwenye ulimwengu wa blogu. Kazi nzuri sana. Nitakuwa mgeni wako hapa kila siku. Harambee!

Post a Comment