Monday, March 28, 2011

Serikali inapokunywa dawa

Kwa kawaida, mawaziri wetu wa Wakuu wa Mikoa wakitoa kauli kuhusu mambo fulani tunasema Serikali imesema au imeagiza. Sasa hivi 'Wakulu wetu' wanamiminika Loliondo kwa Babu kutibiwa, kwa nini tunashindwa kusema "Serikali inaumwa? Kumbuka: Babu alishasema kwake hakuna Kinga, kila anayekwenda anataka Tiba!

Askari Polisi akinywa dawa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akiwa na Rose Nyerere, binti wa Baba wa Taifa, Mwalimu nyerere wakipata Kikombe cha Babu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ezekiel Maige akipata kikombe cha Mchungaji Ambilikile Mwasapila juzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Teresya Huvisa akipata kikombe.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk Yohana Balelel wakipata tiba ya mchungaji Ambilikile Mwasapile wa kijiji cha Samunge, Loliondo juzi.

2 comments:

Anonymous said...

Kimsingi serikali inaumwa, hata kama si magonjwa tunayojua. lazima kuna tatizo linaloifanya isiendelee. Na hilo ndio ugonjwa wake mkubwa

Anonymous said...

Hayo ni matatizo binafsi ya viongozi wa serikali yatofautishwe na serikali yenyewe.

Post a Comment