Tuesday, March 29, 2011

Pia tujifunze kufikiria kinyume


Baada ya taarifa ya serikali hapo jana kueleza kuwa dawa ya Babu wa kule Samunge haina madhara, wengi wamefurahi, hasa wale waliopata kikombe.

Fikra kinyume inahoji, je, ingekuwaje kama ingebainika kuwa dawa hiyo inayotokana na mti wa Mugariga ina madhara kwa binadamu ambayo labda yangejitokeza baada ya muda mrefu?

Fikiria kwamba kila siku anatibu watu 2,000 (kama alivyodai) zidisha mara siku 180 (tangu Oktoba alipoanza) utapata= watu 360,000 (waliokunywa). Hivi hao, ndugu zao, marafiki zao wangekuwa katika hali gani?


Na tushukuru dawa hiyo iwe kweli imetoka kwa Mungu, kama sivyo hali itakuwaje hapo baadaye, baada ya 'NGUVU' iliyoitoa kubainika?

Kwa upande wa serikali iliyoamua 'kutibiwa' na kuivaa dawa hiyo kichwa kichwa, kana kwamba serikali inaongozwa kwa ndoto na utabiri, itakuwa na kauli gani?

Tafakari. Chukua hatua!

No comments:

Post a Comment